Zana ya Rasilimali

Saidia Hoosiers kwa Kuhamasisha Watu Kuhusu 988

Ni muhimu kwetu sote kushiriki ujumbe wa Nambari ya Dharura ya 988 ya Kuzuia Kujiua na Matatizo katika kaunti zote 92 za Indiana. Tumetengeneza nyenzo zifuatazo ili zikusaidie kutangaza ujumbe wa 988 kwa marafiki zako, familia yako, wanachama wako, na washikadau wako. Unaweza kupakua na kutumia maudhui na nyenzo za ujumbe zilizo hapo chini kueneza ujumbe huu muhimu. Nakili tu na ubandike violezo vya barua pepe, nakala ya ujumbe na michoro ili usaidie kuhamasisha watu katika jimbo nzima. Angalia tena mara kwa mara kwani nyenzo za ziada zinatengenezwa.

Kwa rasilimali za kitaifa, tafadhali tembelea zana za SAMHSA.

Nakala ya Barua Pepe

Unaweza kutumia nakala ifuatayo unapotuma barua pepe ili uwaarifu Hoosiers kuhusu Nambari ya dharura ya 988.

Mada: Saidia kuhamasisha watu kuhusu Nambari ya Dharura ya 988 ya Kuzuia Kujiua na Matatizo

Mpendwa [name],

988 inakusaidia kujua mambo ya kutenda. Unapata mtu anayekuelewa na kukupa usaidizi unaohitaji usiohukumu. Unapata chochote unachohitaji, unapohitaji.

988 inatoa muunganisho wa moja kwa moja kwa huduma na usaidizi wenye huruma na rahisi kwa mtu yeyote anayepitia dhiki inayohusiana na afya ya akili, iwe ni mawazo ya kujiua, shida ya afya ya akili au ya matumizi ya dawa za kulevya, au aina nyingine yoyote ya dhiki ya kihisia.

Ili kusaidia kueneza ufahamu wa Nambari ya Dharura ya 988 ya Kuzuia Kujia na Matatizo Usimamizi wa Huduma za Familia na Jamii wa Indiana umeunda nyenzo zinazokufaa. Unaweza kupata nyenzo hizo hapa.

Ikiwa wewe au mtu unayemjua anakabiliwa na tatizo linalohusiana na afya ya akili au matumizi ya dawa za kulevya, matumaini na usaidizi unapatikana. Tafadhali piga simu au utume ujumbe kwa 988 ili ufikie Nambari ya Dharura ya Kuzuia Kujiua na Matatizo na uzungumze na mtaalamu aliyefunzwa kuhusu matatizo saa 24/7.

Asante!

Nakala ya Ujumbe

Unaweza kutumia nakala ifuatayo unapotuma ujumbe ili uwaarifu Hoosiers kuhusu Nambari ya Dharura ya 988 ya Kuzuia Kujiua na Matatizo.

Iwapo wewe au mtu unayemjua kwa sasa ana mawazo ya kujiua au tatizo la afya ya akili au matumizi ya dawa za kulevya, tafadhali piga simu au utume ujumbe kwa 988 ili ufikie Nambari ya Dharura ya Kuzuia Kujiua na Matatizo na uzungumze na mtaalamu aliyefunzwa kuhusu matatizo. 988 inakusaidia kujua mambo ya kutenda na ni usaidizi usiokuhukumu unaoweza kupata unapouhitaji.

Nakala ya Mitandao ya Kijamii

Tumia nakala iliyo hapa chini ili uambatishe picha kwenye mitandao ya kijamii.

Chaguo la 1

Je, 988 ni nini?

988 inakusaidia kujua mambo ya kutenda. Sikio la kusikiliza. Mwanzo wa kupata msaada. Mtu anayekuelewa. Unapata chochote unachohitaji wakati hujui unachohitaji. Piga simu au utume ujumbe kwa Nambari ya Dharura ya 988 ya Kuzuia Kujiua na Matatizo ikiwa wewe au mtu unayemjua anapitia shida inayohusiana na afya ya akili.

Chaguo la 1

Je, 988 ni nini?

988 ni rahisi kukumbuka na zaidi. Inatoa muunganisho wa moja kwa moja kwa huduma na usaidizi wenye huruma na rahisi kwa mtu yeyote anayepitia dhiki inayohusiana na afya ya akili, iwe ni mawazo ya kujiua, wasiwasi, mfadhaiko au shida ya matumizi ya dawa za kulevya, au aina nyingine yoyote ya dhiki ya kihisia.

Michoro: 1080 x 1920

Michoro ifuatayo ya mitandao ya kijamii hutumiwa vyema kama Hadithi za Instagram au Facebook. Bofya kulia (au Control+Click kwenye Mac) kwenye picha iliyo hapo chini ili uihifadhi kwenye kompyuta yako.

Michoro: 1080 x 1080

Michoro ifuatayo ya mitandao ya kijamii hutumiwa vyema kwenye Instagram au Facebook. Bofya kulia (au Control+Click kwenye Mac) kwenye picha iliyo hapo chini ili uihifadhi kwenye kompyuta yako.

Michoro: 1200 x 675

Michoro ifuatayo ya mitandao ya kijamii hutumiwa vyema kwenye Twitter. Bofya kulia (au Control+Click kwenye Mac) kwenye picha iliyo hapo chini ili uihifadhi kwenye kompyuta yako.

Mabango Yanayochapishika

Chaguo zifuatazo za bango na vipeperushi vimeundwa ili uweze kuchapisha na kushiriki. Bofya kwenye picha hapa chini ili kupakua toleo la PDF la kurasa.

Pata msaada sasa.

Iwapo wewe au mtu unayemjua kwa sasa ana mawazo ya kujiua, au tatizo la afya ya akili au matumizi ya dawa za kulevya, tafadhali piga simu au utume ujumbe kwa 988 ili ufikie Nambari ya Dharura ya Kuzuia Kujiua na Matatizo na uzungumze na mtaalamu aliyefunzwa kuhusu matatizo saa 24/7.